LEO NAMLETA KWENU JUSTINO WA CUCAS BEAT INTERNATIONAL
Leo pia ni siku, na kama ni siku ngoja nikujuze hii.
Leo namleta kwenu mtu muhimu kwenye sanaa yetu hapa nchini, na dunia nzima.
Jamaa anajulikana kwa jina la Justin Everest, a.k.a Justino. Huyu jamaa nimeamua nimlete kwenu ili mpate kujua vitu alivyonavyo na kama kuna anachoweza kukusaidia basi usisite kumcheki. Jamaa ni mzaliwa wa nchini Tanzania ukanda wa kaskazini, na makazi yake kwa sasa ni mjini Arusha,
Ngoja niende kwenye lengo, sio siri jamaa amebeba vingi kichwani mwake, Mimi binafsi nilimjua miaka ya nyuma wakati anatoa remex ya nyimbo ya kigoma all star leka dutigite na kuipa jina la kiroba, katika nyimbo hiyo yeye ali compose beat na melody zote mbali na ku compose hiyo beat aliweza kuimba kwa kuigiza baadhi ya sauti za wasanii walioimba kwenye leka dutigite. Mbali na hiyo ameshafanya hits songs nyingi ulizowahi kuzisikia na zingine ambazo hujazisikia. Hivyo jamaa ni producer lakini pia ni mwimbaji pia anauwezo wa kurap.
Kipaji cha tatu kutoka kwa uyu jamaa ni kuwa na uwezo wa kupiga picha nikiwa namaana ni photographer.
Kipaji kingine kutoka kwa Justino ni video director na video editor.
Kingine kutoka kwake ni radio presenter mzuri na kwa sasa anapiga mzigo mambo jambo radio.
Pia jamaa ni events planer na amewahi kushiri kuandaa baadhi ya matamasha kama liliofanyika mwishoni mwa mwaka jana katika uwanja wa sheikh abeid stadium, lililopewa jina la funga mwaka la kaskazini likiwashirikisha wasanii wa ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, na kufana sana.
Kwa mawasiliano na mahojiano nae waweza kumcheki kupitia number hii
0764962493
![]() |
| Justin Everest |

Umetriiiii sha brooo @foe nomakweliii
ReplyDeleteamina kaka
Delete